![]() Nadharia hii inaelezea udumishaji wa uwezo na mamlaka ya tabaka moja kuu juu ya tabaka dogo kwa kutumia mikakati anuwai. ![]() Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hejemonia ilioasisiwa na Antonio Gramsci katika makala aliyoyaandika akiwa gerezani kati ya mwaka wa 1923 na 1936. Hivyo, utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ujitokezaji wa hejemonia katika safu ya hejemonia ya jamii kwa mujibu wa riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Ingawa wahakiki wengi wa riwaya wameweza kuangazia masuala ya kila nui kuhusu asasi za kijamii, suala la hejemonia katika taasisi hizo lilihitaji kumulikwa. Licha ya ubayana wa hali hii katika jamii, watafiti na wahakiki wa tanzu za fasihi andishi hususan riwaya hawajaonyesha namna hejemonia inajitokeza katika asasi za kijamii. ![]() Asasi za kijamii kama vile ndoa, shule, vyuo, utamaduni na malezi zinaendelea kushuhudia utawala wa wenye uwezo juu ya wasio na uwezo. Watu wenye uwezo na mamlaka wanatumia madaraka yao kuwatawala wengine kwa vishawishi anuwai.
0 Comments
Leave a Reply. |